Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliougua corona Tanzania wafika 24

101590 Pic+wagonjwa Waliougua corona Tanzania wafika 24

Wed, 8 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu ametangaza uwepo wa wagonjwa wengine wapya wanne wa maambukizi ya virusi vya corona nchini humo. Waziri Ummy ametangaza leo Jumatatu Aprili 06, 2020 katika taarifa yake kwa vyombo vya habari inayoelezea mwenendo wa hali ya corona nchini Amesema kuwa kati ya wagonjwa hao wanne, wawili wanatoka Tanzania Bara na wawili wanatoka Zanzibar “Wizara ya Afya imethibitisha kuwepo kwa kesi mpya nne za maambukizi ya virusi vya corona (COVI-19) zilizopatikana Dar es Salaam, Mwanza na Zanzibar na kufanya kuwepo kwa jumla ya kesi 24 zilizoripotiwa tangu kuanza kwa ugonjwa huu nchini” imesema sehemu ya taarifa hiyo Amesema kuwa wagonjwa hao wapya ni pamoja na wawili ambao walitolewa taarifa na waziri wa afya Zanzibar jana Jumapili Taarifa hiyo imesema kuwa wagonjwa wawili wa Tanzania Bara wote ni wafanyabiashara na ni raia wa Tanzania ambapo mmoja ni mkazi wa Mwanza aliyewasili kutoka Dubai Machi 24  na mwingine mkazi wa Dar es Salaam. Taarifa hiyo ya waziri Ummy imesema kuwa wagonjwa wote wako chini ya uangalizi wa wataalam wa afya katika vituo maalum vya tiba vya Dar es Salaam, Mwanza na Zanzibar huku wizara ikiendelea kuwafuatilia watu wa karibu waliowahi kukutana na hao wagonjwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz