Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliokiuka uendeshaji salama bohari za kemikali waonywa

F55f12b67b22fb25be338732ebd4d198 Waliokiuka uendeshaji salama bohari za kemikali waonywa

Fri, 4 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe amekemea vikali uendeshaji wa bohari za kemikali usiofuata taratibu na sheria za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Shirika la Viwango nchini (TBS), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) katika uhafadhi wa kemikali wa hizo.

DC Gondwe ameyasema hayo wakati wa ziara yake kwenye Bohari ya kuhifadhi Kemikali ya Junaco Group Ltd katika eneo la Mivinjeni jijini Dar es Salaam ambapo ametoa wito kwa Taasisi hizo kufuatilia Bohari kama hizo kuhakikisha wanafuata sheria ili kuwalinda wananchi haswa wenye makazi katika eneo hilo.

“Wafanyabiashara wa hizi kemikali kwa kweli hatujui zikikaa vibaya hatuwezi kujua kabisa kama zimeharibiaka au kutoboka wapi, zinaweza kuleta madhara kama, na maradhi mbalimbali kwa jamii,” amesema Gondwe.

Kwa upande wake, Meneja wa Kanda ya Mashariki waMaabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Gerald Mollel amesema wamegundua mambo ambayo hayaendani na matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Kemikali nchini, kuchanganya kemikali hizo sehemu ambazo sio sawa, baadhi ya Kemikali kuisha muda wa matumizi.

Mollel amesema kutokana na uwepo wa bohari hiyo Kemikali hizo zinaweza kuleta madhara kama kusambaa na kusababisha magonjwa ya saratani, vipindupindu na magonjwa ya tumbo.

Naye Ofisa Mkaguzi Mwandamizi wa TBS, Mhandisi Donald Manyama amekiri kuwepo sehemu kubwa ya Kemikali hizo kupitwa na wakati (Expired) lakini zinaendelea kuonekana katika sehemu hiyo.

Mwakilishi wa Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Temeke, Joseph Paul amewataka wafanyabiashara wanaofanya biashara hizo za Kemikali kufuata na kuzingatia taratibu za nchi ikiwemo kufuata weledi katika

Chanzo: habarileo.co.tz