Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliokacha ARV kusakwa

Arv Pic Data Waliokacha ARV kusakwa

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani wamemuomba Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuwatafuta watu 68 katika eneo hilo wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) ambao hawatumii dawa za kufubaza virusi hivyo

Hivi karibuni Waziri Ummy alisema watafanya mchakato ili kuwatafuta watu 200,000 nchini waishio na VVU bila kujitambua.

Alisema Tanzania inakadiriwa kuwa na watu milioni 1.7 wanaoishi na VVU, lakini wanaotambua hali zao za afya ni milioni 1.5 pekee.

Akizungumzia hali hiyo jana, Habiba Athuman ambaye ni mkazi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, alisema Serikali inapaswa kuwasaka na kuwapa elimu ili waweze kuwanusuru ambao hawajapata maambukizi.

Alisema kitendo cha mtu kupima na kujua hali yake kinapaswa kupewa elimu sahihi ili imsaidie kwa kuanza dawa za kufubaza virusi hivyo.

Mratibu wa Ukimwi Manispaa hiyo, Dk Lusungu Mselela alisema kuwa watu 68 katika halmashauri hiyo wameacha kutumia dawa ya kufubaza virusi baada ya kupima na kugundulika kuwa na ugonjwa huo.

Alisema katika upimaji huo watu 23,270 walipima VVU na waliogundulika ni 714, kati yao wanawake ni 458 wenye umri chini ya miaka 25 na 90 wapo chini ya miaka 15.

Alisema kuwa hadi sasa watu 638 wamekubali kupata dawa, huku watu 68 hawajakubali wala hawajapenda kutumia dawa.

Dk Mselela alisema hilo ni kundi kubwa, kwa hiyo linapotumia dawa linaleta nguvu ya kuendelea na uzalishaji mali.

“Wapo mabinti wenye chini ya miaka 15, wengi wao wamezaliwa nao, wapo wanaotumia dawa za kufubaza virusi lakini wapo ambapo hawatumii,” alisema Dk Mselela.

Alisema kwa sasa wanapambana ili kila anayepata virusi apate matibabu. Dk Mselela alizitaja sababu za kundi la wasichana kuwa wengi ni kutokana na kukabiliwa na ushawishiwa kutoka kwa watu wazima, kukosa maarifa ya kujikinga na umaskini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live