Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliojeruhiwa kwa Mtume Mwamposa waruhusiwa kutoka hospitali

94420 Majeruhi+pic Waliojeruhiwa kwa Mtume Mwamposa waruhusiwa kutoka hospitali

Wed, 5 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Watu 14 kati ya 16 waliojeruhiwa katika kongamano wa Mtume na Nabii Boniface Mwamposa lililosababisha vifo vya watu 20, wameruhusiwa kurejea nyumbani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Februari 4, 2020 ofisa muuguzi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Kilimanjaro, Josephine Kimario amesema wawili bado wanaendelea na matibabu.

'Tulipokea majeruhi 16 ila wawili wamebaki wanaendelea na matibabu. Hawa waliobaki muda wowote wanaweza kuruhusiwa,” amesema Josephine.

Watu hao walikufa wakati wakigombea kukanyaga mafuta yanayotajwa kuwa na upako mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo Jumamosi iliyopita Februari Mosi, 2020.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz