Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliochukuliwa sampuli ya kupimwa corona wako salama

99580 CORONA ARUSHA+PIC Waliochukuliwa sampuli ya kupimwa corona wako salama

Fri, 20 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Watu 27 ambao walikuwa wamechukuliwa sampuli za vipimo vyao vya afya ili kuwachunguza kama wameambukizwa ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama corona wapo salama.

Mkurugenzi msaidizi kitengo cha ufutiliaji wa magonjwa ya mlipuko wa Wizara ya Afya, Dk Janeth Mghamba akiwa na mtaalam wa majanga wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Faraja Msemwa wametoa taarifa hiyo leo.

Wakizungumza na wanahabari katika jiji la Arusha, wataalam hao wa afya wamesema watu hao walichukuliwa sampuli baada ya kubainika walikutana na dereva wa teksi ambaye alimbeba magonjwa wa corona. "Watu hawa walikuwa karibu na dereva na baada ya kuchukuliwa vipimo na kupelekwa maabara kuu iliyopo jijini Dar es Salaam wamebainika hawajaambukizwa."

Hata hivyo, Dk Mghamba amesema washukiwa hao wataendelea kufatiliwa hadi vitakapofanyika vipimo mara tatu kama ambavyo WHO imeagiza. Dk Msemwa kwa upande wake amesema hadi sasa Mkoa wa Arusha hauna mgonjwa mwingine wa corona zaidi ya Isabella Mwampamba ambaye anaendelea vizuri.

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo amewataka wakazi wa Arusha kuondoa hofu ya ugonjwa huo lakini kuendelea kuchukua tahadhari.

Chanzo: mwananchi.co.tz