Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waliochanjwa Uviko-19 wafikia asilimia 15

Chanjo  Ed Waliochanjwa Uviko-19 wafikia asilimia 15

Thu, 2 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amezindua mpango harakishi wa utoaji wa chanjo ya Uviko-19 (Global Vax), akisema tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipozindua chanjo hizo Julai 2021 ni asilimia 15 tu ya Watanzania ndio wamechanja.

Akizungumza leo Juni 2 katika uwanja wa Mwembeyanga jijini Dar es Salaam, Waziri Ummy amesisitiza kuwa bado ugonjwa huo upo na kuna uwezekano wa kupata wimbi la tano.

“Tangu chanjo imezinduliwa tumeweza kuwachanja, Watanzania milioni 4.6 sawa na asilimia. Wizara tumeweka malengo ifikapo Desemba tuwe tumepata idadi kubwa ya Watanzania walio chanja.

“Leo tunazindua mpango mkakati wa “Global Vax” ilikuweza kuwatayarisha Watanzania kupambana na wimbi litakalokuja,” amesema.

Waziri Ummy, ameeleza katika wiki tano zilizopita wameweza kutambua kunaongezeko kubwa la ugonjwa wa Uviko-19 katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, hususani nchi za kusini mwa Afrika

Hata hivyo, ameeleza kutokana na mwingiliano wa kibiashara baina ya Tanzania na nchi nyingine, Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais (Tamisemi) wameongeza nguvu na jitihada za kukabiliana na Uviko-19. 

Advertisement “Serikali kupitia Wizara ya Afya na kushirikiana na ofisi ya Rais Tamisemi tumeongeza nguvu na jitihada za kukabiliana na Uviko-19 kwa kuwa nchi yetu ipo kwenye hatari ya kukabiliana na wimbi la tano la Uviko-19,” amesema

 “Serikali kwa kushirikiana na wadau wetu, Shirika la Afya duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (Unicef) tumeweza kufikia idadi ya kuwa na vituo 7,000 vya kuchanja kutoka vituo 550 Julai 2021,” amesema.

Amesema Serikali imeidhinisha aina tano za chanjo zitumike nchini ambazo ni Janssen, Pfizer, Modern, Sinopharm, na Sinovac.

“Chanjo hizi zimedhibitika kwamba ni salama, zina ubora na ufanisi katika kuwakinga wananchi kupata ugonjwa wa uviko-19 na zimeidhinishwa na shirika la afya duniani,” amesema

Pamoja na hayo, amesema pia Tanzania imepata msaada wa chanjo kutoka serikali ya Marekani, dozi milioni 13.4 ambapo kati ya hizo, dozi milioni 5 tumezipokea kutoka Ubalozi au Serikali ya Marekani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live