Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Waliochanja wasiogope kufanyiwa tafiti" - Wizara ya Afya

MAKUBI WEB Watanzania waliochanja watakiwa kuondoa hofu wanapofanyiwa utafiti

Thu, 28 Oct 2021 Chanzo: Mwananchi

Serikali imeanza mchakato wa utafiti wa kuwapima afya baadhi ya watu waliopata chanjo ya kuzuia Uviko-19 ili kujua maendeleo ya afya zao.

Lengo la utafiti huo ni kubaini mwenendo wa afya za waliochanjwa ili kuona wastani wa kinga zao na namna wanavyoweza kujikinga.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Oktoba 27, 2021 jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Profesa Abel Makubi wakati akitoa taarifa kuhusu hatua za utekelezaji wa miradi ya afya kwa maendeleo.

Utafiti huo utafanyika kwa kutumia sehemu ya Sh1.3 trilioni ambazo zilitolewa na Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) kwa ajili ya mapambano ya Uviko-19.

Katibu Mkuu amesema katika utafiti huo watapata ukweli wa maendeleo kwa waliopata chanjo wastani wao katika maendeleo ya afya na kama kunahitajika kujikinga zaidi.

Amewataka Watanzania kutokuwa na hofu katika utafiti huo kwani hauna nia mbaya zaidi ni maboresho juu ya kinga na yatakwenda kuwa msaada zaidi kwa wananchi.

"Tunaweza kukuta mfano mtu ana kinga kwa asilimia 70 au 80, hivyo sisi tutajua sasa mtu huyo tumsaidiaje ili kufikia asilimia 100 ya kinga yake, watu wasihofu hata kidogo," amesema Profesa Makubi.

Kauli ya Katibu imekuja huku Serikali ikitangaza kuwa chanjo ya awamu ya kwanza ya Johnson & Johnson zaidi ya dozi milioni moja zimekwisha na sasa Watanzania wanachanja aina ya Sinopharm ambayo imetoka nchini China.

Chanzo: Mwananchi