Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Walimu Zanzibar watakiwa kushauri wanafunzi kuhusu VVU

6befdb84831c4d98ecefe30763e0b6ae Walimu Zanzibar watakiwa kushauri wanafunzi kuhusu VVU

Sat, 12 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Hamasa imetolewa kwa walimu visiwani Zanzibar kutoa ushauri mzuri kwa wanafunzi utakawasaidia kuwaongoza kwenye maisha yao ikiwemo kufahamu namna nzuri ya kujikinga na maambukizi mapaya ya Virusi vya Ukimwi (VVU).

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Dk Idrissa Muslimu Hija alipokuwa anafungua mafunzo ya afya ya uzazi, jinsia pamoja na Ukimwi kwa walimu wa madrasa ya Msingi na kati na sekondari mjini Unguja.

“Mnatakiwa kutoa ushauri kwa upole kwa wanafunzi wenu ili waweze kujikinga na maambukizi mapaya ya virusi vya Ukimwi ili wawe na weledi wa kutosha ni namna gani wanaweza kupambana na ugonjwa huo,” amesema Hija.

Chanzo: habarileo.co.tz