Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakwe kuingizwa katika bima ya afya kwa wote

Bima Ya Afya Kwa Wote Wakwe kuingizwa katika bima ya afya kwa wote

Mon, 23 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, amesema katika Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote, Serikali inapendekeza  wakwe kuingizwa katika bima hiyo.

Akizungumza na wahariri pamoja na viongozi wa dini, jijini Dar es Salaam, leo Jumatatu, tarehe 23 Januari 2023, Serikali imeweka pendekezo hilo kutokana na ongezeko la uhitaji wa wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuwaunganisha wazazi au wakwe zao katika bima za afya.

Ummy amesema kuwa, bima ya kaya inachukua wategemezi sita, ikiwemo mke, mume, watoto na wazazi wa mwanachama.

“Wategemezi tuseme watakuwa sita, maana yake mchangiaji na mwenzake wake na watoto wanne, hatuwezi kuacha bima ikawa na watu 10 au 20, hivyo mwenyewe ataangalia katika watu sita kama utamuweka mama yako mzazi  au mkwe,” amesema Ummy.

Ummy amesema “tumeona watu wanawatoa watoto zao wanaingiza wazazi au wakwe sababu wanaumwa sana, anamtoa mtoto sababu haumwi sana anataka kumuingiza mzazi au mkwe. Tumeangalia tunavyoanza tunataka kuvutia watu.”

Waziri huyo wa afya amesema, katika muswada huo, Serikali inapendekeza bima ya kaya ya watu sita gharama yake iwe 340,000 kwa mwaka. Pia, inapendekeza kitita cha mafao ya msingi chenye gharama ya 66,000 ambapo wahusika watapa huduma za msingi za afya katika vituo vya afya, zahanati na hospitali za Serilkali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live