Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakurugenzi sekta ya afya watakiwa kufuata miongozo ya manunuzi

Mqku Prof Makubi amewataka watumishi hao kutofanya kazi kwa mazoea

Thu, 31 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakurugenzi wa taasisi na wa Hospitali za rufaa za mikoa wametakiwa kufuata miongozo na sheria za manunuzi ili kuondoa hati chafu na zenye mashaka kwenye taasisi zao.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya afya Prof. Abel Makubi wakati akiendesha mkutano wa baraza kuu la wafanyakazi wa Wizara ya afya lililofanyika jijini Dodoma.

Prof. Makubi amesema ni viongozi wanatakiwa kuwa mfano katika utekelezaji wa majukumu yao mahali pa kazi kwa kufuata miongozo na sheria ya manunuzi ya bidhaa kwa ajili ya mahitaji ya ofisi au ujenzi pamoja na maboresho ya miundombinu ya hospitali zao ili kuondokana na hati chafu au zenye mashaka.

Aidha, Prof. Makubi amewataka waganga wafawidhi wa hospitali za Rufaa za Mikoa kuhakikisha wanasimamia upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba kwenye hospitali zao.

“Ifike muda kila mgonjwa anayefika kwenye hospitali yako uhakikishe anapata dawa zilizopo kwenye mwongozo wa dawa (STG). Tunataka malalamiko yanayotolewa na wananchi yapungue ikiwemo ukosefu wa dawa pamoja na kutopata huduma kwa wakati”. Amesema Prof. Makubi.

Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo aliwakumbusha viongozi hao pindi wanaporudi kwenye vituo vyao vya kazi kuwakumbusha madaktari walio chini yao kuandika dawa zilizopo kwenye muongozo huo na wahakikishe dawa wanazoziagiza ni zile ambazo zipo kwenye muongozo.

Prof. Makubi amewataka watumishi hao kutofanya kazi kwa mazoea na wanatakiwa kufanya kazi kulingana na kasi ya utendaji wa viongozi waliopo na kutekeleza majukumu wanayopangiwa kwa weledi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live