Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakazi Dar kupimwa afya zao bure

Tue, 5 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuanzia kesho Jumatatu Februari 4, 2019 watapata fursa ya kuchunguzwa afya zao bure katika shughuli itakayofanywa na timu ya madaktari wa Hospitali ya Kairuki.

Shughuli hiyo itakayofanyika katika viwanja vya Mbagala Zakhiem itakuwa ya siku tatu ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha mwanzilishi wa hospitali hiyo Hubert Kairuki.

Ofisa uhusiano wa hospitali hiyo, Arafa Juba akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Februari 3, 2019 amesema shughuli hiyo itahusisha upimaji wa virusi vya Ukimwi, saratani ya matiti na kifua kikuu.

Amesema wanawake watakaobainika kuwa na dalili za saratani ya matiti watapata nafasi ya kufanyiwa uchunguzi wa kina kwenye hospitali hiyo.

“Kwa kawaida kipimo cha kubaini saratani ya matiti kinagharimu kati ya Sh80,000 hadi Sh100,000 lakini watakaoonekana kuwa na dalili watafanyiwa bure, hivyo ni nafasi nzuri kwa wanawake wa Dar es Salaam,” amesema.

“Tumeona tufanye saratani ya matiti kwa sababu ni tatizo linalowasumbua wanawake wengi. Na kwa kiasi kikubwa wengi hawajitambui mapema,” ameongeza.



Chanzo: mwananchi.co.tz