Wauguzi katika chuo cha afya cha Kozhikode wakiendelea na matibabu" /> Wauguzi katika chuo cha afya cha Kozhikode wakiendelea na matibabu"/> Wauguzi katika chuo cha afya cha Kozhikode wakiendelea na matibabu"/>

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakati Tanzania tukijilinda na Ebola, ugonjwa mwingine hatari zaidi duniani unaoenezwa na popo waibuka

8244 DdspnNIVQAA9dl2 TZW

Tue, 22 May 2018 Chanzo: bongo5.com

height="400" class="wp-caption-text">Wauguzi katika chuo cha afya cha Kozhikode wakiendelea na matibabu

Kwa mujibu wa maafisa wa afya katika jimbo la Kerala lililopo kusini mwa nchi hiyo, wamethibitisha vifo vya watu 6 mpaka sasa mmoja akiwa ni Nesi aliyekuwa akiwahudumia waathirika kutokana na kinachodhaniwa kuwa ni virusi vya Nipah, huku watu wengine 26 wakilazwa kwa matibabu na uchunguzi wa kitaalamu.



Ugonjwa huo unaoenezwa na POPO ni miungoni mwa orodha ya magonjwa 10 hatari zaidi ya milipuko ambayo yanaangaziwa zaidi na Shirika la Afya Dunia (WHO).

Tayari Waziri wa Afya nchini India, Jagat Prakash Nadda ameagiza mamlaka husika mjini Kerala kufunga maeneo yote yenye mikusanyiko ya watu ikiwemo Waranti ili kuzuia maambukizi zaidi ya virus hivyo vya Nipah.



Dalili za mtu aliyeambukizwa virusi vya Nipah.

->Homa kali ya mwili

->Maumivu ya kichwa

->Uchovu na usingizi mzito

-> Kupumua kwa tabu na kuchanganyikiwa.

Mpaka sasa hakuna chanjo ya ugonjwa huo.

Loading...
Chanzo: bongo5.com