Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wajawazito wapata ahueni huduma za afya

Dcccc Wajawazito wapata ahueni huduma za afya

Thu, 22 Jul 2021 Chanzo: ippmedia.com

Wanawake hao wanatoka katika vijiji vya Misayu, Ihata, na Mwadui mkoani Shinyanga.

Walibainisha hayo juzi wakati wadau wa maendeleo kutoka kampuni za ununuzi wa zao la tumbaku  kutoa Sh. milioni 464 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama,  Festo Kiswaga.

Fedha hizo zilitolewa kwa ajili ya ujenzi wa zahanati na ununuzi wa vifaa tiba katika  hafla iliyofanyika kwenye Kijiji cha Misayu.

Mmoja wa wanawake hao,  Ester Bundala, alisema wajawazito wengi kwenye vijiji hivyo wanajifungulia majumbani kutokana na ukosefu wa huduma ya afya.

‘Tunapojifungulia  nyumbani kwa kuzalishwa na wakunga wa jadi huwa tupo katika hatari kubwa ya kupoteza maisha, sababu wao hawana vifaa maalum vya kuhudumia mjamzito hasa pale unapomwaga damu nyingi au kuhitaji kujifungua kwaupasuaji, matokeo yake mzazi anafariki,”  alisema Bundala. 

Naye Mariamu Masunga kutoka Kijiji cha Misayu,  alipongeza kutolewa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa zahanati, ambayo itawasogezea huduma karibu.

Naye Meneja mradi kutoka kampuni ya Tambuka,  Osca Luoga, alisema ujenzi huo wa zahanati kwenye kijiji hicho cha Misayu, utakuwa msaada kwa vijiji hivyo.

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Wilaya ya  Kahama (KACU),  Emmanuel Charahani, alisema wataendelea kuzihimiza kampuni zingine za ununuzi wa zao hilo  kurudisha sehemu ya faida wanazozipata kwa kuwatatulia wananchi kero mbalimbali ikiwamo sekta ya afya, elimu na maji.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama,  Festo Kiswaga, alisema kampuni hiyo imekuwa na uzalendo  kwa kurudisha faida kwa wananchi kutatua kero zao, huku akiwataka wanawake kuacha kujifungulia majumbani ili kupuguza vifo vya mama na mtoto vitokana na uzazi.

Chanzo: ippmedia.com