Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wajawazito walalama kutopewa huduma stahiki kwenye zahanati

MIMBA W Wajawazito walalama kutopewa huduma stahiki kwenye zahanati

Sat, 7 Jan 2023 Chanzo: ippmedia.com

Waliwasilisha malalamiko hayo wakati wa mkutano wa hadhara wa mbunge wa jimbo hilo, Mussa Sima aliyekuwa kwenye ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo.

Mmoja wa wakazi wa Kijiji hicho, Saidoro Mangu, alidai kinamama wajawazito wanaokwenda kufuata huduma za kujifungua nyakati za usiku wamekuwa hawapati mapokezi sahihi kutoka kwa watoa huduma wa zahanati hiyo.

"Kutokana na kinamama hao kutopata mapokezi rafiki kutoka kwa watoa huduma wa zahanati hiyo wamekuwa wakijifungulia nje ya zahanati hiyo kutokana na watoa huduma hao kutowajali kinamama hao.

"Hii inauma sana kwani mimi mwenyewe niliwahi kushuhudia tukio moja lililotokea katika zahanati hiyo la mama mjamzito kujifungulia nje ya zahanati kutokana na watoa huduma waliokuwapo kituoni hapo kutowajali wateja wao waliowaweka hapo," alidai.

Alisema kuwa wakati umefika kwa serikali ya wilaya hiyo kupitia kwa mwakilishi wa wananchi na Mkurugenzi kuangalia upya utendaji wa watoa huduma walioko kwenye kituo hicho kwani inawezekana wamekaa muda mrefu na kujikuta wakitawaliwa na mazingira.

Aliyekuwa Diwani wa Mtipa, Saidi Chima alionyesha masikitiko yake kwa wananchi wa kijiji hicho kutoshirikishwa katika kufanya uamuzi wakati wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Alisema anafahamua kuna baadhi ya watu hawatakiwi kuonekana katika shughuli za maendeleo kwa madai kuwa anapinga maendeleo ya kijiji hicho.

"Kwa nini tupinge maendeleo, hatupingi tu maendeleo kwani tunahoji tujue kinachoendelea, kwani tungejua Sh. milioni mbili zimejenga ofisi na sisi tumepatiwa kiasi hicho cha fedha unafikiri kuna mtu angehoji? Chima aliuliza.

Akijibu malalamiko ya wananchi hao, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Jeshi Lupembe, alikiri kupokea malalamiko hayo na tayari ameshamwandikia barua ya kumsimamisha kazi Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho hadi uchunguzi utakapokamilika.

"Na kwa sababu mimi ninasimamia ilani ya uchaguzi, kero hii mlivyosema, mimi nilishaletewa ofisini kwangu, na nilishamwita WEO (Ofisa Mtendaji wa Kata), na hatua nimeshachukua ya kumwandikia baru na kuanzia kesho hatakuwa hapa," alisema.

Mbunge Sima aliwaahidi wakazi wa kijiji hicho kwamba kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa, wataunda timu ya kwenda kuchunguza kama tuhuma za watoa huduma wa zahanati hiyo zina ukweli au la.

Mussa ambaye kitaalumu ni mwalimu, alisisitiza kwamba endapo timu hiyo itabaini kinamama wajawazito kutopatiwa huduma zinazostahili, serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria watoa huduma hao.

"Limejitokeza jambo kama hili kule Sokoine, sisi tumeliona kwenye vyombo vya habari, changamoto imejitokeza na timu imeundwa ya wilaya, Mkurugenzi umeunda timu, timu imeundwa ya mkoa na timu imeundwa ya kitaifa.

"Tunatarajia ndani ya wiki hii tutapata majibu hatua zitakazochukulia katika hospitali yetu," alisema.

Chanzo: ippmedia.com