Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wajawazito 309, vichanga 1,200 wamepoteza maisha 2022

Mimba D Watoto Wajawazito 309, vichanga 1,200 wamepoteza maisha 2022

Tue, 17 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Akina Mama wajawazito 309 na watoto wachanga 1,200 wamepoteza maisha katika kipindi cha mwaka 2022 katika kanda ya Mashariki nchini Tanzania, Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Zuwena Jiri amesema.

Akifungua kikao kazi cha tathimini ya mwaka na mapitio ya vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto chini ya miaka mitano kanda ya Mashariki, Zuwena amesema bado kuna changamoto.

"Takwimu hizi hazifurahishi hivyo kikao kazi hiki kitumike vizuri katika kufundishana, kubadilishana mawazo na kupanga mikakati ambayo itatusaidia katika kuhakikisha tunaboresha huduma za Afya ya uzazi na watoto wachanga katika kanda yetu ya Mashariki,” amesema Jiri

Jiri Amesisitiza kuwa matatizo yanayochukua uhai wa wapendwa wetu yanaweza kuzuilika kwa asilimia 95 kama tukijipanga vyema toka kwa mama anapokuwa mjamzito.

"Tuipe elimu jamii yetu ili wajue umuhimu wa wajawazito kuwahi kliniki mapema ikiwa chini ya wiki 12 kwa lengo la kujikinga yeye pamoja na mtoto na kama kuna hatari inayotaka kujitokeza basi iwahiwe mapema." Amesema Jiri

Chanzo: www.tanzaniaweb.live