Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wajasiliamali wa kemikali watakiwa kujisajili

534e6e3aeab1d4ae9cf26e6755e524f0 Wajasiliamali wa kemikali watakiwa kujisajili

Tue, 2 Mar 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKEMIA Mkuu wa Serikali, Dk Fidelis Mafumiko amewataka wajasiriamali wanaojihusisha na biashara za kutumia kemikali kuhakikisha wanafuata taratibu na kujisajili.

Rai hiyo alitoa wakati wa mafunzo wa siku moja iliyohusisha wajasiriamali wadogo kutoka mikoa ya kanda ya ziwa wanaotumia kemikali katika shughuli zao.

Dk Mafumiko alisema wajasiliamali wanatakiwa kutumia kemikali kwa kufuata utaratibu. Alisema wajasiriamali wengi wanatakiwa kujisajili kupitia Shirika la kuhudumia viwanda vidogo(SIDO) ambapo gharama ni 110,000/-.

Alisema kupitia mafunzo hayo wajasiliamali watajengewa uelewa juu ya matumizi salama ya Kemikali. Amewataka Wajasiliamali kuhakikisha wanaepuka kuhifadhi kemikali hatarishi kama petroli au mafuta yanayowaka ndani ya nyumba.

Alisema wajasiriamali waache tabia ya kuchanganya tindikali pamoja na maji kutokana na kufanya hivyo ni makosa. Meneja wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo(SIDO) mkoani Mwanza,Bakari Songwe alisema wataendelea kutoa mafunzo ya uchakataji wa kemikali.

Alisema SIDO wataendelea kushirikiana na Taasisi zilizobobea katika masuala ya kemikali. Songwe alisema kwa mkoa wa Mwanza ndani ya miaka mitano 2015-2020 wamefanikiwa kusajili viwanda vidogo vya wajasiliamali 2000. Mjasiriamali wa sabuni za maji, Grace Florence ameiomba Serikali iwe inatoa mafunzo hayo mara kwa mara.

Alisema bado changamoto ni kubwa sana mitaani kutokana na watu wengi wamekuwa wajasiriamali wa sabuni na hawajui jinsi ya kuandaa pamoja na kutengeneza sabuni hizo. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia mkuu wa Serikali(GCLA) Mwanza

Chanzo: habarileo.co.tz