Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahudumu wa afya 184 wapatiwa usafiri

Pic Pikipiki Wahudumu wa afya 184 wapatiwa usafiri

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wahudumu wa afya 184, Maofisa afya saba na Maofisa Maendeleo ya Jamii wawili wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza wamekabidhiwa pikipiki na baiskeli ili kuongeza ufanisi wa kazi zao.

Wahudumu hao wa afya kutoka vijiji 73, mitaa na vitingoji 419 katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema wamekabidhiwa baiskeli zenye thamani ya Sh46 milioni, Maofisa afya wakikabidhiwa pikipiki zenye thamani ya Sh7.9 milioni zikiwa ni fedha za mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (SRWSSP) na pikipiki mbili zilizokabidhiwa kwa Maofisa Maendeleo ya Jamii zikitoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu.

Akikabidhi vyombo hivyo vya usafiri, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Yusta Mwambembe amewataka watoa huduma hao kuhakikisha wanavitumia vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuweza kuleta matokeo chanya katika shughuli za usafi wa mazingira pamoja shughuli za Maendeleo ya Jamii.

“Mlikuwa na changamoto ya usafari sasa changamoto hiyo imetatuliwa nendeni mkatekeleze majukumu yenu Kwa weledi ili mkaisadie jamii,”amesema Mwambembe

Mratibu wa mradi wa Usafi wa Mazingira vijijini , Abdulahman Mgonja amesema pikipiki na baiskeli hizo zitaleta matokeo chanya kutokana na watoa huduma hao kukabiliwa na changamoto za usafiri mara kwa mara wanapohitaji kufanya shughuli za usimamizi wa usafi na mazingira.

Amewataka watumishi hao pamoja na wahudumu wa afya kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kufikia malengo ya mradi huo sambamba na kuboresha mazingira kuwa safi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live