Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wahudumu afya wapigwa msasa

11595 Wahudumu+pic TanzaniaWeb

Tue, 17 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bahi. Ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga, Serikali kwa kushirikiana na shirika lisilo la Serikali la World Vision imetoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika wilaya za Chemba na Bahi mkoani Dodoma.

Wahudumu wa afya 66 kutoka tarafa za Mundemu wilayani Bahi na Sanzawe, Chemba wamepata mafunzo namna ya kumhudumia mjamzito na mtoto mchanga hadi atakapofikia miaka mitano.

Vijiji 24 vitafikiwa na huduma hiyo vikiwamo vijiji 13 kutoka Bahi na 11 vya Chemba.

Akifunga mafunzo wilayani Bahi juzi, meneja wa World Vision Kanda ya Kati, Faraja Kulanga alisema yamelenga kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga. “Tathmini iliyofanyika ilionyesha tarafa za Mundemu na Sanzawa zilikuwa na idadi kubwa ya vifo vya wajawazito na watoto wachanga, tukaamua kuleta mradi huu wa miaka mitano tuna hakika utaleta mabadiliko makubwa,” alisema Kulanga.

Naye meneja mradi wa afya ya mama na mtoto wa World Vision, Noel Mbanguka alisema changamoto kubwa inayowakabili wahudumu wa afya wakati wa kutekeleza majukumu yao ni kutopewa ushirikiano wa kutosha kutoka kwa walengwa hasa wanaume.

Chanzo: mwananchi.co.tz