Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagonjwa wa figo waongezeka Muhimbili

Prof. Janabi Muhi Profesa Mohamed Janabi.

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi amesema kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa Figo ambapo ameongeza kwa siku hospitali hiyo inahudumia Wagonjwa 120 hadi 130.

Profesa Janabi ameihimiza jamii kuchukua tahadhari na kufuata mtindo bora wa maisha na kusisitiza kuwa vitu hatari zaidi kwa afya ya mwili ni sukari na wanga na wala sio mafuta kama wengi wanavyodhani.

Profesa huyo aliongeza kuwa mwili hautunzi wanga wala sukari, badala yake huvibadilisha kuwa mafuta, hivyo, amewataka watu kupunguza matumizi ya vyakula vyenye sukari na wanga.

“Sukari ni ugonjwa hausababishwi na fangasi na bacteria, unasababishwa na lishe, lazima tubadilishe mtindo wa maisha, mtakaopata nafasi mzungumze na mtu anayefanyiwa dialysis (kusafisha figo) ndio mtafahamu umuhimu wa kutunza figo,” amesema Janabi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live