Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagonjwa wa TB waongezeka Zanzibar

Wagonjwa TB Wagonjwa wa TB waongezeka Zanzibar

Thu, 24 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati kesho ikiwa maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu (TB) Duniani imelezwa kuwa hali ya ugonjwa huo visiwani Zanzibar imeongezeka kutoka idadi ya wagonjwa 1,074 kwa mwaka 2020 hadi wagonjwa 1,090 mwaka 2021.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Hassan Hafidh wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.

Amesema kuongezeka kwa ugonjwa huyo ni kutokana na baadhi ya watu kushindwa kufika katika vituo mbali mbali vya afya wakati wanapoona hali zisizokua za kawaida.

Amesema anaamini kuwa iwapo jamii ingekua na mazoea ya kufika vituo vya afya bila shaka wagonjwa wangebainika mapema na kupewa matibabu.

Hata hivyo akiendelea kufafanua zaidi alisema jukumu la wananchi kujitokeza hospitali kupima afya zao si la Serikali pekee bali wananchi wenyewe wanapaswa kujiwekea utaratibu huo kila mara.

Akitaja baadhi ya dalili za maradhi hayo amesema ni pamoja na kukohoa kwa muda mrefu, kupatwa na homa za masaa hasa wakati wa jioni pamoja na kutokwa na jasho lisilokua la kawaida.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live