Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagonjwa upasuaji wa ubongo waongezeka

Yy Wagonjwa upasuaji wa ubongo waongezeka

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daktari Bingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Henry Humba, amesema wagonjwa wanaohitaji huduma ya upasuaji wa ubongo, mishipa na mifupa ya fahamu imeongezeka kutokana na mfumo wa maisha unavyobadilika hasa kwa nchi zinazoendelea.

Dkt. Humba ameyasema hayo leo Julai 21, 2022, Jijini Dodoma mara baada ya kukutana na wataalamu wa upasuaji wa viungo vya binadamu ikiwemo nyonga, mifupa, mishipa ya fahamu na ubongo kutoka Hospitali ya kibingwa ya Apollo nchini India, kwa lengo la kubadilishana ujuzi wa kibingwa katika sekta ya afya kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Kwa upande wake Daktari bingwa wa mfumo wa fahamu ,nyonga na ubongo kutoka Hospitali ya Apollo India Dkt.Ruthiramurthy Irish, amesema wamekuja Tanzania kubadilishana utaalamu wa kibingwa bobezi wa mifupa kwa kuwa ni moja ya nchi inayoonekana kufanya vizuri pindi inaposhirikishwa katika sekta ya afya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live