Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagonjwa kutoka nje waongezeka Ocean Road

70f816b50401882c5bf2a261d4ac68eb Wagonjwa kutoka nje waongezeka Ocean Road

Sat, 5 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk. Julius Mwaisalage amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan, idadi ya wagonjwa wanaotoka nje ya nchi kutibiwa katika taasisi hiyo imeongezeka.

Dk. Mwaisalage amesema awali walikuwa wanapokea wagonjwa 70 hadi 80 kwa mwaka, lakini sasa wamefikia wagonjwa 124.

Amesema ongezeko la wagonjwa hao ni baada ya kuwepo kwa matibabu ya kibingwa.

"Mashine ya Pet CT-scan, ni mradi mkubwa wa kimkakati, ambao ulianza awamu ya tano, lakini ukamilishaji ni mwaka huu

“Ujenzi wa jengo ulianza mwezi Juni mwaka jana na utekelezaji utafanyika mwezi Machi mwaka huu, na mashine zitasimikwa hadi mwezi Juni,” amesea.

Mkurugenzi huyo ameeleza mafanikio mengine ni uboreshaji wa tiba mionzi, mashine za linex ambayo ni za kisasa zinatoa huduma za mionzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live