Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagonjwa 78 wapandikizwa figo Tanzania

4aa157d88ecd14e371df665e040a7b89.png Wagonjwa 78 wapandikizwa figo Tanzania

Fri, 12 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAGONJWA 316 wamepandikizwa figo katika hospitali mbalimbali hadi kufikia Novemba mwaka jana wakiwemo 78 waliopta tiba hiyo kwa madaktari wazawa katika hospitali za hapa nchini.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima aliyasema hayo jana jijini Mbeya wakati akitoa tamko la maadhimisho ya siku ya figo duniani yatakayofanyika leo.

Dk Gwajima alisema Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa sugu wa figo kati ya 4,800 na 5,200 wanaohitaji huduma ya kusafisha damu au kupandikizwa figo na kati ya hao 1,000 wanapata huduma ya usafishaji wa damu.

Alisema wagonjwa 78 wamepandikizwa figo na madaktari wazawa wakiwemo 62 waliopata tiba hiyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na 16 hospitali ya Benjamin Mkapa 16. Dk Gwajima alisema, wagonjwa wengine walipata tiba hiyo nchini India.

Alisema mpango wa wizara ni kuhakikisha inaziwezesha hospitali zote 26 za rufaa za mikoa ili ifikapo mwaka 2025 zitoe huduma za tiba ya ugonjwa sugu wa wa figo ikiwa ni pamoja na kusafishaji damu.

"Wagonjwa wa figo ni kati ya wagonjwa walio katika hatari kubwa ya maambukizi ya magonjwa ya mfumo wa hewa kama vile kifua kikuu na bakteria hivyo ni muhimu kuendelea kuielimisha jamii kujikinga na madhara ya magonjwa ya kuambukiza." Alisema Dk Gwajima.

Alisema lengo la serikali ni kuwapunguzia wagonjwa gharama za tiba kwa kuwasogezea huduma kwenye mikoa yao kuliko kuendelea kugharamia nauli na fedha za kujikimu wakiwa ugenini.

"Tumeongeza huduma za kibingwa katika hospitali zetu ambapo kwa sasa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, hospitali zote za rufaa za kanda na hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga ya Bombo zinatoa huduma ya usafishaji damu kama tulivyoshuhudia katika Hospitali ya Kanda ya hapa Mbeya."alisema Dkj Gwajima.

Alilitaja kundi la wanaume kuwa sehemu ya waathirika wakubwa wa ugonjwa wa figo ikilinganishwa na wanawake hatua aliyosema inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mfumo uliojengeka kwa kundi hilo kutopendelea kupima afya zao mara kwa mara na baadaye wanajitokeza tatizo likiwa limekuwa.

Mratibu wa huduma za Figo kutoka wizara ya Afya, Dk Linda Ezekieli alitoa mwito kwa jamii izingatie ushauri wa wataalamu kuhusu kujikinga na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kupata lishe bora, kufanya mazoezi sambamba na kuzingatia uwiano wa uzito na kimo cha mwili ili kuepuka uzito uliopitiliza.

Aliwasihi pia wanaume wabadilike na kupenda kupima afya akisema ni wakati kwao kutambua kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuzijua dalili za matatizo ya kiafya kabla ya kufikia hatua ya tiba.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya, Dk Godlove Mbwaji alisema hospitali hiyo imekuwa ikipokea wagonjwa mbalimbali kutoka mikoa inayoihudumiwa na kwa wale wanaohitaji huduma ya matibabu katika ngazi za juu imekuwa ikitoa rufaa huku pia ikiendelea kuwafuatilia.

Chanzo: www.habarileo.co.tz