Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagonjwa 250 walioshindwa kulipia gharama za matibabu waruhusiwa

Thu, 4 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nairobi, Kenya. Zaidi ya wagonjwa 250 ambao wameshindwa kulipa gharama za matibabu wameruhusiwa kurudi nyumbani nchini Kenya.

Wagonjwa hao waliokuwa wamelazwa Hospitali ya Kenyatta walikuwa wamezuiliwa baada ya kushindwa kulipa gharama zao za matibabu.

Hospitali hiyo imekana madai kwamba baadhi ya wagonjwa walikuwa wamezuiliwa kinyume na matakwa yao japokuwa taarifa za ndani zinaeleza kuwa ni kawaida kwa hospitali hiyo kuwazuia wagonjwa kuondoka hadi walipe gharama zao za matibabu.

Uchunguzi  uliofanywa na televisheni ya The Citizen nchini Kenya umefichua suala  hilo na kubaini kwamba baadhi ya waliokuwa wakizuiliwa katika hospitali hiyo ni wanawake ambao wamekumbwa na matatizo baada ya kujifungua.

Lakini hospitali hiyo inasema kwamba iliwaruhusu  wagonjwa 250  katika kipindi cha wiki mbili, ikiwamo 52 ambao waliruhusiwa.

Msemaji wa Hospitali hiyo, Hezekile Peter amekana kwamba wagonjwa hao walikuwa wakizuiliwa.

Amesema wagonjwa  hao waliachiliwa baada ya kukubali kulipa gharama za matibabu baada ya kurudi katika shughuli zao za kawaida.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz