Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagonjwa 200 waliolazwa MOI wasaidia, wito watolewa

Wagonjwa 200 waliolazwa MOI wasaidia, wito watolewa

Mon, 10 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wagonjwa zaidi ya 200 wanaohudumiwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) Dar es Salaam nchini Tanzania wamepatiwa msaada wa vitu mbalimbali vinavyoweza kuwasaidia wakati wakipatiwa matibabu.

Msaada huo wenye thamani ya Sh3.8 milioni umetolewa na ‘MySaccos’ chama cha watu walio na asili ya Mkoa wa Njombe waishio jijini Dar es Salaam na mikoa mingine ni sabuni, pampasi za wakubwa na watoto, mafuta, juisi, maji, nguo

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo leo Jumapili Februari 9, 2020 mwenyekiti wa Mysaccos, Fredrick William amesema licha ya kutoa msaada kwa wagonjwa wanaopatiwa matibabu MOI lakini pia wamejipanga kutoa misaada katika hospitali nyingine.

“Misaada hii inahitajika katika sehemu mbalimbali na malengo yetu ni baadaye kwenda katika taasisi ya Saratani (Ocean Road) kwa sababu pia wanahitaji misaada hii,” amesema Fredrick William

Mbali na kutoa misaada hiyo pia ametoa rai kwa watu binafsi, taasisi na mashirika mbalimbali kutoa misaada ya vitu kwa wagonjwa na watu wasiojiweza.

Kwa upande wake, Muuguzi mkuu kiongozi wa zamu wa MOI, Zaituni Bembe amesema msaada huo utawasaidia wagonjwa wengi huku akiwataka watu wengine kujitoa.

Pia Soma

Advertisement
“Wengi wamekuwa wakija kutuona na kutupatia msaada tunawashukuru sana lakini mahitaji bado ni mengi ikiwamo ya madawa na pampasi za wakubwa na wadogo hivyo tunaomba watu waendelee kutuunga mkono,” amesema Zaituni.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz