Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagonjwa 120 wafanyiwa operesheni bila kufungua fuvu

85c7acef80c8420691abc8b49aaa3763 Wagonjwa 120 wafanyiwa operesheni bila kufungua fuvu

Wed, 9 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) ya Dar es Salaam imefanya upasuaji wa ubongo bila kufungua fuvu kwa zaidi ya wagonjwa 120 katika mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dk Respicious Boniface alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati akieleza mafanikio ya taasisi hiyo katika mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita.

Alisema kuwa kabla ya mashine ya kupasua bila kufungua fuvu (Angio Suite), wagonjwa walikuwa wanapelekwa nje ya nchi huku gharama za matibabu zikiwa ni Sh milioni 30 hadi 60 lakini hapa nchini huduma hiyo ni Sh milioni 10 hadi 15.

Dk Boniface alisema kuwa kupitia huduma hiyo wagonjwa wamekuwa hawakai muda mrefu hospitalini hivyo gharama zinapungua. Mashine hiyo iligharimu Sh bilioni 7.9 na huduma ilianza kutolewa Januari 26, 2021.

“Zamani kabla ya kuanza kufanya upasuaji huu ulikuwa unafungua ili ufike inachukua saa sita kwenye ubongo sasa unatumia saa moja hadi moja na nusu,” alisema na kuongeza kuwa mgonjwa anakuwa hana kidonda kikubwa hivyo anakaa muda mfupi.

Gharama yake nje ya nchi ni Sh milioni 40 lakini ndani ya nchi ni Sh milioni nane.

Alisema mafanikio mengine ni ununuzi wa mashine sita za kusaidia kupumua na vitanda 12 vya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) kupitia fedha za mgawo wa Covid-19.

Ufungaji wa mashine kwa ajili ya kupasua bila kufungua fuvu (Angio Suite) uligharimu kiasi cha Sh bilioni 7.9 ambapo huduma hiyo ilianza kutolewa Januari 26, 2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live