Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waganga Wakuu nchini waagizwa kuharakisha vyeti vya waliochanja

SUBI Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Dr. Leonard Subi

Fri, 20 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imeagiza waganfa wakuu wa mikoa yote nchini kuhakikisha wanaingiza taarifa za waliopata chanjo ya Corona kwenye mfumo wa taarifa za kielektroniki mpaka kufikia August 25, 2021.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Dr. Leonard Subi imeeleza kubwa waganga wakuu wote nchini wanatakiwa taarifa za waliopata chanjo kwenye fomu maalumu na kuzituma taarifa hizo wizarani ili taarifa hizo ziweze kuandaa vyrti vya kielektroniki kwaajili wananchi wote waliopata chanjo kwenye vituo 550 nchi nzima.

Dr. Subi ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akijibu swali la waandishi waliotaka kujua uwepo wa tofauti za vyeti kwa wananchi waliopata chanjo za Corona nchini.

Dr. Subi amesema kuwa kwa wale waliopata chanjo na wanahitaji kusafiri nje ya nchi wakiwa nav yeti vya chanjo wanatakiwa kwenda kwenye vituo walivyopatia chanjo wakiwa na taarifa za safari zao na watapatiwa vyeti vya kielektroniki.

Amesema mpaka sasa jiji la Dodoma limeshatumia chanjo 12, 000 kati ya 50,000 zilizotolewa na Wizara ya Afya na tayari kuna vituo 28 kwaajili ya wanaohitaji chanjo hizo.

Mapema jana wananchi waliofika kupata chanio wamekiri kupata vyeti vya kielektoniki muda mfupi tu baada ya kuchanja na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupata chanjo hiyo.

Ally Hamis ni mmoja wa wananchi waliofika kupata huduma hiyo "Nilienda kuangalia kama cheti change kimeshakua tayari, lakini baada ya kufika nimekuta cheti cha kielektroniki kiko tayari na ndani ya dakika 1o tu nikakipata.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live