Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafungwa, mahabusu kuanza kupimwa TB

70057 Pic+wafungwa

Mon, 5 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania kupitia Idara ya Kinga-Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu (TB) na Ukoma (NTLP) kwa kushirikiana na idara kuu ya jeshi la Magereza nchini humo imeandaa mafunzo kwa maofisa Magereza kwa ajili ya kufanya mapitio ya kisera na taratibu za kitaalamu za kuchunguza na kudhibiti TB kwa watuhumiwa, mahabusu na wafungwa.

Akizungumza leo Jumatatu Agosti 5, 2019 katika ufunguzi wa mafunzo hayo Meneja wa NTLP, Dk Beatrice Mutayoba amesema tafiti mbalimbali zinaonyesha kuna kiwango kikubwa cha TB miongoni mwa wafungwa wapya na huugua ugonjwa huo kabla ya kutumikia vifungo vyao.

“Matokeo haya yanadhihirisha umuhimu wa kufanya uchunguzi wa TB kabla mfungwa hajaandikishwa gerezani na wakati akiwa anaendelea kutumikia kifungo chake” amesema.

Amesema shughuli hiyo ya kudhibiti TB linalenga kuyajengea uwezo magereza ili kuyaepusha na uwezekano wa kuwa chanzo cha kusambaza maambukizo.

Kwa upande wake, Kamishna wa sheria na uendeshaji wa Magereza Tanzania, Uwesu Ngarama ameshukuru Serikali kwa kazi hiyo ya kudhibiti TB katika magereza mbalimbali hapa nchini.

“Tunashukuru kuingia katika mpango huu ambao utatusaidia kutatua changamoto za TB ili kuimarisha afya za mahabusu na sisi pia kwa sababu ni watu ambao tunaishi kwa pamoja kila siku,” amesema.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz