Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafanyakazi Chuo Kikuu Mount Meru waiangukia Serikali

27264 Chuo+pic TanzaniaWeb

Thu, 15 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Wafanyakazi 82 wa Chuo Kikuu cha Mount Meru Arusha wameitaka Serikali kuingilia kati ili walipwe stahiki zao kiasi cha Sh1.1 bilioni.

Wakizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Novemba 15, 2018 wafanyakazi hao wamesema uongozi wa chuo hicho kinachomilikiwa kwa sasa na Kanisa la Baptisti Tanzania unawataka kuondoka chuoni.

Mwenyekiti wa wafanyakazi wa chuo hicho, Michael Sambu amesema kwa miezi 10 sasa hawajalipwa mishahara.

"Tunadai malimbikizo ya mishahara Sh435.4 milioni, likizo Sh110.8 milioni na pensheni Sh579.6 milioni," amesema

Makamu mwenyekiti wa wafanyakazi hao, Christian Charles amesema pia wanaomba Serikali kuingilia kati kujua nani mmiliki wa chuo hicho.

Amesema hivi sasa kuna mgogoro wa umiliki wa chuo ambao unachangia wafanyakazi kukosa haki zao.

Chuo Kikuu cha Mount Meru, hivi karibuni kimesitishiwa kudahili wanafunzi na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutokana na kushindwa kufikia vigezo.



Chanzo: mwananchi.co.tz