Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau watahadharisha; waliomaliza darasa la saba hatarini kukeketwa

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam Wasichana kutoka koo 12 za Wilaya ya Tarime waliohitimu darasa la saba mwaka huu wapo hatarini kukeketwa.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 6,  katika Mkutano ulioandaliwa na Mtandao wa Jinsia(TGNP) kwa kushirikana na  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA)  uliohusisha mashirika saba ya  kutetea  na kulinda watoto wa kike dhidi ya ukatili.

 Akizungumza katika mkutano huo, Meneja Mradi kutoka taasisi ya kuzuia ukeketaji ya ATFGM Valerian Mgani amesema wamejiandaa vyema kuhakikisha wanawapa hifadhi kwenye kambi zilizoandaliwa ili kuwanusuru na visu vya ghariba.

“Kwa kawaida koo hizo hufanya ukeketaji kwa mwaka ambao unagawanyika, wasichana wanaomaliza darasa la saba ndiyo wamekuwa wakitumika kama chambo, kila koo unachagua wasichana 10 na kuwapeleka kukeketwa ikiwa ni hatua ya maandalizi ya Desemba,”amesema Mgani.  

Amesema ikitokea mmoja amekufa basi huaminika kwamba mizimu ya ukoo husika imekasirika hivyo na kawaida desemba ndiyo mwezi ambao ukeketaji hufanyika.

“Tumejiandaa kuwapokea kwenye kambi zetu, tumeweza kuwaepusha wengi kufanyiwa kitendo hicho cha kikatili, mwaka 2014 tuliwanusuru 636, mwaka 2016 wasichana 365 walikimbilia kujificha kwenye kambi yetu hivyo kusalimika,” amesema  

Mwenyekiti wa Sauti ya Jamii Kipunguni Selemani Bishagazi amesema  kuwa taasisi yao baada ya kutambua kwamba ukeketaji umefanywa kama chanzo cha kipato, wameandaa mafunzo ya ujasiriamali ili kubadili fikra.

Mratibu kutoka Idara ya ujenzi wa nguvu za pamoja TGNP Mtandao Grace Nsetu amesema wamekutana kujadili mikakati yao ya kampeni ya kuzuia masuala ya ukeketaji wakishirikiana na UNFPA na wadau wengine.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz