Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau sekta ya afya wakabidhi vifaa tiba, Siku ya mtoto Njiti

Njiti Watoto Wadau sekta ya afya wakabidhi vifaa tiba, Siku ya mtoto Njiti

Wed, 16 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, Doris Mollel Foundation imesema itakabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya Sh180 milioni katika hospitali za Wilaya za Serengeti, Ukerewe, Kwimba, na Magu ili kusaidia kutatua changamoto ya vifaa tiba.

Pia, imesema kuwa inatarajia kufunga wa mitambo ya hewa oxygen kwa watoto wachanga katika hospitali za Siha, Karatu, Monduli na Dabaldi pamoja na kukabidhi mitungi 200 ya gesi yenye Sh 8 milioni kwa ajili ya kina mama wajawazito katika Wilaya ya Serengeti.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Doris Molle huku akiwashukuru wadau wote wa maendeleo kwa moyo wao wa kujitoa na kuwasihi waendelee na moyo wa kutatua changamoto za afya.

Maadhimisho hayo ambayo huadhimishwa mnamo 17 Novemba kila mwaka yatafanyika Wilayani Serengeti mkoani Mara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live