Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waagizaji,wasambazaji wa dawa za binadamu waahidi kushirikiana na JKCI

Moyo Ed Waagizaji,wasambazaji wa dawa za binadamu waahidi kushirikiana na JKCI

Tue, 25 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Kikao hicho kilihudhuriwa na wawakilishi zaidi ya 30 kutoka katika makampuni mbalimbali za dawa.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Prof. Mohamed Janabi, ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo amesema ukikosa dawa za moyo unahatarisha maisha ya mgonjwa hivyo kujenga uhusiano na wadau hao ni jambo la muhimu.

“Kulikuwa na changamoto za mawasiliano, kutokufuatwa kwa taratibu za kuagiza dawa, kutokufahamu maoteo ya dawa sawa sawa, kutoletwa dawa zote kamili kama zilivyoagizwa haya yote tumeyazungumzia na kupata utatuzi. Katika Taasisi yetu hatukuwa na matatizo ya upatikanaji wa dawa kwa asilimia 85, ninaamini baada ya kikao hiki tutakuwa na uhakika wa upatikanaji wa dawa kwa asilimia 100 na mgonjwa atapata dawa zote alizoandikiwa na daktari”.

“Tutakuwa na maoteo ya dawa sahihi zaidi baada ya mazungumzo yetu, kwani ukiwa na dawa za kutosha kwa kipindi cha miezi 3 hadi 4 na ikifika katikati ya miezi miwili ukaagiza zingine una uhakika wa kuwa na dawa za kutosha muda wote. Haya ni baadhi ya mambo ambayo tumekubaliana”, amesema Prof. Janabi.

Chanzo: ippmedia.com