Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WIZARA: Hakuna vifo vya Corona Aprili- Mei 04, 2022

Coronavirus?fit=1600%2C900&ssl=1 Hakuna vifo vya Corona Aprili- Mei 04, 2022

Sat, 7 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Afya inaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu hali ya ugonjwa wa UVIKO-19 nchini ambapo imesema hadi tarehe 04 Mei 2022 kumekuwa na jumla ya Watu 33,916 waliothibitika kuwa na UVIKO-19 na vifo ni 803.

"Idadi ya maambukizi mapya imekuwa ikipungua kutoka 116 kwa mwezi Machi 2022 hadi kufikia 68 katika mwezi Aprili 2022, katika mwezi Aprili 2022, kumekuwa na ongezeko la wagonjwa kutoka Watu nane (08) wiki ya tatu hadi 32 katika wiki ya nne"

"Hakuna kifo chochote kilichotolewa taarifa katika kipindi cha mwezi wa Aprili 2022 hadi tarehe 4 Mei 2022, katika kipindi hiki, Mkoa wa Dar es Salaam umeendelea kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya Watu waliothibitika kuwa na ugonjwa huu (wagonjwa 70) sawa na 87.5% ya wagonjwa wote"

"Mikoa mingine yenye taarifa za wagonjwa wa UVIKO-19 ni pamoja na Arusha (6), Kilimanjaro (2), Morogoro (1) na Mwanza (1), katika kipindi cha tarehe 02 Aprili hadi 4 Mei 2022, jumla ya wagonjwa wapya waliolazwa ni wawili (2) tu, na wote hao walikuwa hawajapata chanjo ya aina yoyote dhidi ya UVIKO-19, aidha katika kipindi hicho, hapakuwa na mgonjwa yeyote mahututi kati ya waliolazwa"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live