Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WHO yatoa tathmini miaka miwili ya Corona Tanzania

CORONA CHANJO?fit=660%2C371&ssl=1 WHO yatoa tathmini miaka miwili ya Corona Tanzania

Tue, 15 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema wakati Tanzania ikitimiza miaka miwili tangu kisa cha kwanza cha Uviko-19 kuripotiwa, mwitikio wa kupamba na ugonjwa huo umeimarika huku waliothibitika kupata maambukizi wakifikia watu 33,773 na vifo 800.

WHO imesema kwa kipindi cha Januari 2020 hadi Desemba 2021 ilipokea jumla ya Dola za Kimarekani milioni 6.6 sawa na Sh152 bilioni kutoka kwa wafadhili mbalimbali zilitolewa kusaidia kupambana na ugonjwa huo.

Machi 16, 2020 Tanzania ilirekodi kisa cha kwanza cha Uviko-19 baada ya mgonjwa wa kwanza kupatikana Arusha kabla ya virusi kusambaa katika maeneo mengine.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne, Machi 15, 2022 na WHO imeeleza kuwa mpaka sasa nchi imerekodi visa 33,773 na vifo 800, kulingana na ripoti ya wizara ya afya Machi 11.

Katika miaka miwili tangu hapo, hatua za afya ya umma, ikiwa ni pamoja na kuboreshwa kwa ufuatiliaji wa watu waliokuwa karibu na wagonjwa, kupima uelewa wa umma kuhusu hatua za kuzuia zimekuwa muhimu katika kupunguza kuenea kwa virusi.

Chanjo pia inaimarishwa ili kusaidia kudhibiti janga hili, kwa lengo la kuchanja asilimia 60 ya idadi ya watu.

Advertisement Mkurugenzi Mkaazi wa WHO Tanzania, Dk Tigest Ketsela Mengestu amesema walipokea Dola za Kimarekani milioni 6.6 sawa na Sh152 bilioni kutoka kwa wafadhili mbalimbali ambazo zimeelekezwa kwenye shughuli mbalimbali za mwitikio ikiwa ni pamoja na uchangiaji wa vifaa, mafunzo ya kada mbalimbali za watumishi wa afya na wasimamizi waafya, na kuajiri wataalam.

"WHO inawashukuru wafadhili tofauti, wadau na wafanyakazi wa afya kwa juhudi ambazo wameweka katika kujenga utayari na kukabiliana na janga hili. Tunatumai kuwa ushirikiano utaendelea tunaposonga mbele na tunatumai kuwa katika siku zijazo Tanzania itachangia kufanya Uviko-19 isiwe tishio kwa afya ya umma," Dk Mengestu.

WHO inaendelea kuiunga mkono nchi kuimarisha hatua muhimu za kukabiliana na janga kama vile ufuatiliaji, upimaji, matibabu, na ushiriki wa jamii.

Amesema katika kipindi chote cha janga hili, shirika pia limetoa miongozo ya kitaalam na msaada na pamoja na washirika wake kuwasilisha vifaa muhimu vya matibabu nchini ili kukabiliana na virusi.

"Tumekuwa mstari wa mbele katika juhudi za kukabiliana na janga hili na tunaendelea kuunga mkono juhudi zote ambazo mamlaka za kitaifa zinafanya ili kukabiliana na UVIKO-19 na kuwaweka watu salama," amesema Dk Mengestu.

Amesema chanjo bado ni silaha yenye nguvu dhidi ya janga hili na kwamba WHO inafanya kazi na washirika ili kuongeza ushamiri wa chanjo nchini.

Dk Mengestu amesema mpaka kufikia sasa watu 2,664,373 wamepatiwa chanjo kamili na juhudi zaidi zinahitajika kufikia idadi kubwa ya watu ili kuwalinda kutokana na hatari ya maradhi makali na vifo vinavyozuilika.

Kupitia ripoti ya hivi karibuni Tanzania, wizara ya afya iliendelea kuonya kila mtu kuendelea kuchukua tahadhari kwa kufuata hatua zote za kujikinga katika maeneo ya umma.

"Miaka miwili iliyopita imekuwa na changamoto nyingi, lakini tumejifunza vitu muhimu katika afya ya umma. Tunaibuka na nguvu zaidi na tunatarajia kuendelea kushirikiana na Serikali kuimarisha na kuboresha mfumo wa afya ili kuwa na uwezo wa kukabiliana na dharura za siku zijazo,” amesema  Dk Mengestu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live