Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WHO yatoa tahadhari nyingine ya Corona

0be08989 002b 401e A0c1 A2b19bedb6ee Corona World 4a321e62 586x394 478x394 WHO yatoa tahadhari nyingine ya Corona

Sat, 11 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania, Dk Tigest Mengestu amewataka Watanzania kusherehekea Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kwa amani huku wakichukua tahadhari dhidi ya Covid-19.

Aliyasema hayo jana wakati akitoa maoni na mapendekezo yake kwa waandishi habari jijini Dar es Salaam juu ya huduma za afya kwa wote na maboresho ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa wote.

“Covid-19 bado ipo na inaendelea kupoteza maisha ya wengi duniani, rai yangu kwenu na umma wa Watanzania tuendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo, mbinu za kujikinga ni zile zile; kutumia vitakasa mikono, maji tiririka, kukohoa kistaarabu, kuvaa barakoa na kuepuka misongamano isiyo ya lazima,” alisema Dk Mengestu.

Akizungumzia hali ya Covid-19 kidunia, Dk Mengestu alisema tangu kugundulika kwa ugonjwa huo hadi sasa takribani watu milioni 266 waligundulika kuambukizwa ugonjwa huo na watu milioni 5.3 wamepoteza maisha duniani kote.

“Jitihada zaidi zinachukuliwa kukabiliana na ugonjwa huu ili kuhakikisha maambukizi yanapungua ama kuisha kabisa ambapo hadi Desemba 6,2021 dozi bilioni 7.952 zilisambazwa duniani kote, tunaendelea kusisitiza tahadhari tajwa hapo juu, hata kama chanjo zinasambazwa duniani kote na kugunduliwa kila siku tusiache kuvaa barakoa haswa kipindi hiki cha sikukuu,” alisema Dk Mengestu.

Aidha, alizungumzia juhudi zinazochukuliwa na serikali ya Tanzania kuhusu NHIF ili bima ya afya iwe kwa wote na namna wabunge walivyochangia Bungeni.

“Tunaamini kuwa huduma ya afya ni moja ya haki za binadamu kwa wote si kipaumbele kwa wenye uwezo tu bali ni suala la wote, hivyo serikali ione ni namna gani itafanikisha jambo hilo kwani watu milioni 100 duniani hawamudu huduma za matibabu kwa hiyo lazima tuwe na mpango utakaoangalia usawa zaidi,” alisema Dk Mengestu.

Kwa upande wake, ofisa wa masuala ya uchumi katika afya wa WHO Tanzania, Maximilian Mapunda, alisema wao wanaangalia zaidi katika mihimili mikubwa mitatu katika kufanikisha azma ya afya kwa wote.

Aliitaja mihimili hiyo kuwa ni kugharamia huduma za afya; uimarishaji wa utoaji huduma za afya; na jinsi wananchi wanavyonufaika na huduma za afya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live