Sat, 23 Jul 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Shirika la Afya Duniani WHO, limeutangaza ugonjwa wa Homa ya Nyani "Monkeypox" kuwa dharura ya afya ya dunia.
Kwa uamuzi huo sasa inamaanisha kuwa WHO inachukulia mlipuko huo kama tishio kubwa kwa afya ya dunia ambapo suluhisho la haraka linatakiwa kupatikana.
Mpaka sasa nchi za Ulaya ndio kitovu cha mlipuko huo, na kwa mujibu wa tafiti wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja wapo hatarini zaidi.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live