Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WHO sio ya kawaida

Ndui Ugonjwa wa ndui

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Afya Duniani (WHO) limethibitisha watu 780 walioambukizwa ugonjwa wa ndui usio wa kawaida katika nchi 27 ulimwenguni ambazo kwa kawaida hazijawahi kuwa na ugonjwa huo wa ndui ya nyani unaofahamika kwa kimombo kama MonkeyPox.

Takwimu za hivi punde hazijumuishi maambukizi katika nchi za Kiafrika ambazo kwa kawaida hukumbwa na maradhi hayo.

Katika taarifa yake shirika la WHO limesema kwa sasa, hatari ya afya ya umma katika ngazi ya kimataifa inatathminiwa kuwa ya wastani ukizingatia hii ni mara ya kwanza kuripotiwa kwa virusi hivyo.

Hakuna aliyefariki kati ya watu hao 780 walioambukizwa. Mpaka sasa watu 66 wamekufa katika nchi tano za Afrika kutokana na ugonjwa wa ndui ya nyani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live