Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WHO imeanza uchunguzi juu ya uwepo wa kirusi kipya cha Corona

MAABARAAA WHO imeanza uchunguzi juu ya uwepo wa kirusi kipya cha Corona

Wed, 1 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Afya Duniani (WHO) imeanza kufanya uchunguzi juu ya aina moya ya kirusi cha Corona kinachojulikana kama “”Mu” ambacho kiligunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Columbia mwezi January 2021.

WHO wamesema kuwa kirusi hicho kina tabia ya kujibadili hivyo kuongeza hatari ya kuwa na nguvu zaidi ya chanjo za Corona hivyo bado shirika linafanya tafiti zaidi kuweza kujua na kuelewa namna nzuri ya kupambana nacho.

Kumekua na hofu kubwa baada ya kuwepo kwa aina mpya za virusi vya corona pamoja na kuongezeka kwa maambukizi mapya duniani nzima, mbali na maambukizi ya kirusi cha Delta ambacho kimeongeza kasi ya kusambaa kwa maambukizi hasa kwa watu ambao hawajapata chanjo.

Kirusi hiki kipya kimeongeza hofu kutokana na usambaaji wake kuwa wa haraka na rahisi, na imeelezwa kuwa watu wanaoambukizwa kirusi hiki wamekua kwenye hatari kubwa kwasababu kirusi cha “Mu” hakisikii dawa, chanjo wala tahadhari zozote.

Mpaka sasa WHO imeshatambua aina 4 za virusi tofauti ikiwemo Alpha ambacho kipo nchi 193 na Delta ambacho kipo nchi 170.Virusi vingine aina 5 bado viko kwenye uchunguzi ikiwemo kirusi cha “Mu”.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live