Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WHO: Visa viwili vya ugonjwa hatari 'Marburg' vyarekodiwa

MARBUGGGGGG.png WHO: Visa viwili vya ugonjwa hatari wa 'Marburg' vyarekodiwa

Fri, 8 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WHO imetuma timu ya wataalam nchini humo ili kusaidia wahudumu wa afya wa kujiandaa kwa uwezekano wa mlipuko baada ya kurekodi visa viwili vya virusi vya Marburg, ugonjwa wa kuambukiza ulio familia moja na virusi vya Ebola, baada ya majibu ya vipimo vya awali kutoka kwa wagonjwa wawili waliofariki

Mwakilishi wa WHO nchini humo, Dkt. Francis Kasohole amesema kuwa wagonjwa hao walionyesha dalili za kuhara, homa, kichefuchefu na kutapika na sampuli za vipimp vyao hizo zimepelekwa katika Taasisi ya Pasteur nchini Senegal kwa uchunguzi zaidi

Inaelezwa kuwa virusi vya Marburg huambukizwa kwa watu kutoka kwa popo wa na huenea kati ya wanadamu kupitia maji maji ya mwili na hadi sasa hakuna chanjo ya virusi hivyo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live