Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WHO: Tunahitaji Tsh. Trilioni 45 ndani ya miezi 12 kupambana na COVID-19 duniani

AAQ6Nlu.jfif Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus, ambaye ni Mkurugenzi wa WHO

Sun, 31 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Afya Duniani WHO, limesema kuwa ndani ya miezi 12 ijayo linahitaji zaidi ya Tsh. Trilioni 45 ili kuweza kupambana na janga la COVID-19.

Taarifa hii imetolewa na Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus, ambaye ni Mkurugenzi wa WHO wakati wa Mkutano wa Viongozi wa nchi 20 Tajiri Duniani uliofanyika Roma nchini Italia. Guteres amesema kuwa nchi Tajiri zinapaswa kulipa kiasi hicho ili kusaidia nchi masikini katika kupambana na janga la Corona.

Kwa mujibu wa Guteres kiasi hicho cha pesa kitasaidia gharama za kununua na kutunza chanjo za Corona, kununua vipimo na matibabu ili kusaidia kupunguza athari za vifo duniani kote.

Mpaka sasa Bara la Afrika limetoa chanjo kwa asilimia 10 tu ya wananchi wote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live