Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WHO: Omicron inaua ni hatari

Omicron Kenya WHO: Kirusi cha Omicron hakipaswi kuainishwa kama hakina makali, kinaua watu

Fri, 7 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Visa Milioni 9.5 vimeripotiwa ulimwenguni Wiki iliyopita, ikiwa ni ongezeko la 71%.

Japokuwa Kirusi cha Omicron kimeonekana kutosababisha makali kama Delta, WHO imesema Kirusi hicho hakipaswi kuainishwa kama 'Hakina makali'.

Mkuu wa Shirika hilo, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kama ilivyokuwa kwa aina zilizopita, Omicron inapelekea watu kulazwa na inaua. Pia, kasi ya idadi kubwa ya maambukizi inapelekea Mifumo ya Afya kuzidiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live