Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WHO "Hakuna dalili za corona kumalizika 2021"

Screenshot 2021 03 03 At 10.18.58 660x400.png WHO "Hakuna dalili za corona kumalizika 2021"

Wed, 3 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

Nchi mbalimbali zinapambana kuhakikisha raia wake wanapata chanjo ya Covid-19 wakati janga la virusi vya Corona likiendelea.

Shirika la afya duniani (WHO) linasema janga hilo halina dalili ya kumalizika mwaka huu.

WHO linaamini kwamba janga la virusi vya corona halina uwezekano wa kumalizika katika miezi ya karibuni.

Mkurugenzi wa Mpango wa dharula wa shughuli za kiafya WHO, Michael Ryan, amesema anadhani ni mapema kufikiria kwamba watalimaliza janga hili kufikia mwishoni mwa mwaka.

Amesema kinachoweza kumalizwa ikiwa ulimwengu utakuwa makini ni idadi ya watu kulazwa hospitali kutokana na virusi hivyo au vifo na matatizo mengine yanayosababshwa na janga hilo.

Aidha, WHO imetoa wito kwa Nchi mbalimbali kujiepusha kuondoa haraka shughuli za kudhibiti virusi vya corona, kutokana na kuwepo chanjo.

FISI 22 WAUAWA, WAMEUA WATU WATANO, MAMA AMWAGA MACHOZI “LIFISI LIMEKULA MTOTO WANGU”

Chanzo: millardayo.com