Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WHO: Asilimia 95 waliopata chanjo kutougua Corona

6ea4efce8bdb7e5e084a1ae7b6f02fd6 WHO: Asilimia 95 waliopata chanjo kutougua Corona

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

CHANJO ya Corona imeelezwa kuwa na ufanisi mkubwa kwa asilimia 95 kwa mtu aliyechoma tofauti na asiyechomwa.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Mpango wa chanjo wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini, Dk William Mwengee, ambaye alisema mtu aliyepata chanjo ana asilimia 95 ya kutopata ugonjwa huo ukilinganisha na ambaye hajapata chanjo.

“Chanjo ni salama na zimeweza kuzuia maambukizi kwa wale waliopata chanjo, mtu ambaye hajapata chanjo uwezekano wake wa kukigwa ni mdogo sana asilimia 5 tu,” alisema Mwengee

Naye Mkurugenzi mkazi wa shirika hilo nchini, Dk. Tigest Ketsela Mengestu, amewatoa hofu watanzania kuhusu chanjo ya Covid 19 inayoendelea kutolewa nchini kote.

Dk Mengestu ametumia nafasi hiyo pia kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuonesha mfano wa kupokea chanjo hadharani ambayo amesema mwitikio wake umekuwa mzuri miongoni mwa wananchi.

Aidha amewatoa hofu watanzania kuwa chanjo zinazotolewa na serikali ni salama kwani moja ya jukumu la shirika hilo ni kufanya ithibati ya ufanisi na usalama wa chanjo za dharura kabla ya kuanza kutumika.

Lakini pia amesisitiza chanjo sio mbadala wa matumizi ya vipukusi, kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji tiririka au kukaa mbalimbali kwenye mikusanyiko.

"Kumekuwa na habari nyingi mitaani kuhusu chanjo ambazo nyingine si za kweli, ni jukumu la waandishi wa habari kupeleka taarifa sahihi kwa jamii ili iweze kuelimika na kujikinga na janga hili linaloisumbua dunia" alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz