Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WFP wasitisha kutoa huduma Uganda

47364 Pic+WFP

Wed, 20 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kampala, Uganda. Shirika la Chakula Duniani (WFP) limesitisha shughuli ya kugawa chakula cha misaada kwa wakimbizi nchini Uganda.

Hiyo ni baada ya madai kuibuka kuwa watu wawili wamefariki na wengine zaidi ya 200 kulazwa katika hospitali ya Karamoja kaskazini mashariki mwa nchi hiyo baada ya kutumia unga wa uji unaodaiwa kuwa na sumu.

Vifo hivyo vilitokea baada ya watu hao kunywa uji wenye lishe maalum waliotayarisha kutokana na msaada wa unga uliotolewa na WFP.

Shirika la msalaba mwekundu limeripoti kuwa waathiriwa wanaonyesha ishara za kuugua ugonjwa wa akili pia.

Kwa mujibu wa WFP familia za waathiriwa zilipokea unga huo wa msaada wiki iliyopita.

Lengo la msaada huo ni kuboresha lishe miongoni mwa akina mama wajawazito na wale wanaonyonyesha, watoto walio kati ya umri wa miezi sita hadi miaka mitano.

Msemaji wa Wizara ya Afya Uganda, Emmanuel Ainebyoona amesema wizara hiyo imechukua sampuli ya watu waliokula chakula hicho kwa uchunguzi zaidi.

 

''Kwa sasa tunasubiri uchunguzi wa maabara ya sampuli zilivyochukuliwa kutoka kwenye chakula kupelekwa maabara ya taifa ya uchunguzi,'' alisema

Ainebyoona pia amesema vipimo vya damu ya wagonjwa waliolazwa vimepelekwa katika mabara kuu kwa uchunguzi kubaini chanzo ni nini.

Hatua nyingine ambayo WFP imechukua ni kwenda kwenye makazi ya waliopewa unga huo warudishe ule waliobakisha huku wakiwahimiza watu kupitia kwa viongozi mashinani wasiendelee kuutumia.

Akina mama wanaonyonyesha wameshuriwa wasiendelee kuwanyonyesha watoto wao.

Uganda inawahifadhi wakimbizi zaidi ya milioni moja wengi wao wanawake na watoto kutoka nchini Sudan Kusini.



Chanzo: mwananchi.co.tz