Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vyuo vinavyofanya udanganyifu kukiona

Header20 Prof Makubi ameonya kutovumilia aina yoyote ya udanganyifu

Tue, 10 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amesema kuwa, Serikali haitaendelea kuvumilia tabia ya udanganyifu unaofanywa na baadhi ya vyuo vya afya nchini, kwani tabia hizo hupelekea kupata Watumishi wasio na ubora na kurudisha nyuma jitihada za Serikali za kuboresha huduma kwa wananchi.

Prof. Makubi amesema hayo leo Mei 10, 2022 wakati akifungua Mkutano wa Wakuu wa vyuo vya afya wenye kauli mbiu "Huduma bora za Afya ni matokeo ya uwepo wa vyuo bora nchini," uliofanyika Jijini Dodoma.

Sambamba na hilo, Prof. Makubi amewaelekeza Wasajili wa Mabaraza ya kitaaluma kuchukua hatua stahiki kwa wakufunzi wanaoshiriki kwenye udanganyifu, kwa kuwafutia leseni na hatua nyingine kwa mujibu wa Sheria za nchi.

Naye,Mkurugenzi wa Mafunzo na rasilimali watu Wizara ya Afya Dkt. Saitore Laizer amemshukuru Katibu Mkuu kwa kuendelea kusaidia vyuo vya mafunzo, na kuahidi kutekeleza maelekezo yote aliyotoa ili kufikia lengo la Serikali la kuboresha huduma kwa wananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live