e wajua? Jina la kisayansi la ndizi ni “Musa”, kutoka kwa familia ya Musaceae ya mimea ya kitropiki inayochanua maua ambayo huonyesha tunda la ndizi lililounganishwa juu ya mmea huo. Ndizi moja iliyoiva ikiliwa, hutoa takriban kalori 110, gramu 0 za mafuta, gramu 1 ya protini, gramu 28 za kabohaidreti, gramu 15 za sukari (iliyotokea kiasili), gramu 3 za Fiber, na miligram 450 za potasiamu.
Ndizi zina potasiamu nyingi, husaidia afya ya moyo na kudhibiti shinikizo la damu. Zikiwa na vitamini C na B6, huimarisha kinga na kusaidia metaboliki ya mwili. Nyuzinyuzi mumunyifu husaidia usagaji wa chakula, na sukari asilia hutoa nguvu ya haraka. Ndizi husaidia na kukuza ustawi wa afya kwa jumla.
Kwa ufupi ni kwamba, kuna baadhi ya watu huwa na mazoea flani ambayo wamejijengea hasa katika utaratibu wa kula vyakula vya kila siku (Asubuhi, mchana na Usiku). Imekuwa ni mazoea ambayo tunayo hasa wakati wa kula vyakula vyetu, na mazoea haya muda mwingi yatahusisha kuchanganya matunda flani ndani ya sahani zetu za vyakula.
Tabia hii au mtindo huu wa kula umekuwa ni mazoea ambayo hupelekea hadi watu wengine kupondea pondea au kukatia katia matunda ndani ya vyakula vyao kama si kula matunda hayo punde baada ya kumaliza kula chakula. Unaweza ukawa si wa kwanza kushuhudia haya kwa mtu aliyeagiza wali, pilau, ugali, ndizi, au chakula chochote kile. Binafsi nimeshuhudia haya yakitendeka na kwa mazoea nami nimekuwa muhanga wa tabia au utaratibu huu wa kuchanganya ndizi au pengine parachichi ndani ya chakula changu. Hakika, tumekuwa tukifurahia michanganinyiko hii kwa tabasamu tunapoitia vinywani mwetu.
Ndizi limekua tunda pendwa kwa ajili ya kuchanganya na aina flani ya chakula. Matunda haya yamesheheni virutubisho muhimu ambavyo hutusaidia kuboresha afya katika miili yetu. Lakini!, vipi ikiwa tafiti za kiafya zitakuambia kwamba kuchanganya ndizi na vyakula fulani kunaweza kuleta matokea mabaya na kuathiri afya yako na ustawi kwa ujumla?
Sasa, Hapa kuna vyakula vitano kama si saba unapaswa kuepuka kuoanisha na ndizi kwa gharama yoyote. Iwe kwa kuchanganya ndizi yako ndani ya vyakula hivi au kula ndizi yako baada ya kumaliza kula vyakula hivi, inapaswa kuepuka kabisa kutumia ndizi na vyakula hivi.
Maziwa na bidhaa za maziwa (Milk and dairy products)
Ndizi kwa asili zimesheheni protini, nyuzinyuzi na madini mengine muhimu kama vile magnesiamu, fosforasi, potasiamu, na vitamini B, ambayo huzifanya kuwa ni tunda lenye ujazo kamili ambao umesheheni lishe tosha. Lakini endapo ndizi zitaunganishwa na mafuta ya maziwa na virutubisho vingine vitakanavyo na maziwa huongeza kiwango cha virutubisho na hufanya iwe vigumu kusaga chakula na mchanganyiko huu unaweza kusababisha kuvimbiwa na tumbo kujaa kitu ambacho kinatesa na kinakunyima uhuru wa kukaa au hata kulala.
Vyakula vyenye Protini nyingi (High protein foods)
Watu wengi hufuata lishe yenye protini nyingi, ambapo huchanganya samaki, nyama au mayai na kula pamoja na ndizi mbivu. Hali hii kwa ujumla inaweza kupunguza kasi ya usagaji na mmeng’enyo wa chakula. Ndizi ni tunda ambalo hupelekea wepesi wa usagaji wa chakula. Sasa, punde utakapo changanya ndizi na vyakula ambayo vina asili ya kuwa na protini nyingi ambavyo usagaji wake huenda taratibu hupelekea matatizo. Vyakula vyote vyenye virutubisho vingi vya proteni (High protein Foods) huyeyuka taratibu mwilini. Inashauriwa si vyema kuvichanganyanya na tunda aina ya ndizi ambalo nalo lina protein kiasi. Utakapo changanya ndizi na chakula chochote chenye nyama nyingi, samaki, mayai, nyama ya kuku, nyama ya nguruwe (Pork), siagi n.k, kunaweza kusababisha kuchacha kwa chakula tumboni na kuleta gesi kali kwenye njia ya usagaji chakula na mara nyingine hupelekea kujihisi kushiba kupita kiasi.
Wanga uliosindikwa (Processed curbs)
Wanga ni moja ya virutubisho ambavyo ni muhimu kwa mahitaji ya nishati ya miili yetu. Wanga ni chanzo muhimu cha lishe bora inayojumuisha utoaji wa nishati muhimu kwa shughuli za kila siku ambazo hutekelezwa na miili yetu. Wanga hupatikana katika vyakula mbalimbali, ikiwa ni pamoja na nafaka, matunda, mboga mboga, na maziwa. Ulaji wa ndizi na vyakula vyenye wanga iliyosindikwa kwa wingi kama vile vitafunio vya sukari, keki (Curbs cake) au bidhaa zilizookwa, ugali, wali, ngano n.k kunaweza kusababisha kuongezeka kwa kasi na kushuka kwa ghafla kwa viwango vya sukari kwenye damu. Hii inaweza kusababisha hisia za uchovu na njaa muda mfupi baada ya kula.
Ndizi ambazo hazijaiva (Green Banana)
Hii inaweza kuonekana kama ni kitu cha ajabu, lakini ndizi mbivu kwa ujumla ni rahisi kusagika zikiliwa, lakini kuzioanisha na ndizi mbichi (Hasa zilizopikwa) kunaweza kusababisha usumbufu wa usagaji chakula kwani ndizi mbichi huwa na wanga unaostahimili kwa kiasi kikubwa (More resistant starch), ambayo inaweza kuwa ngumu kusagika na inaweza kusababisha kuvimba kwa tumbo na kuonekana kubwa sana baada ya kula ndizi zilizopikwa kwa kuchanganya na ndizi mbivu, kwa wengine mchanganyiko huu wa chakula huleta gesi na watu wengi huishia kupumua (Kujamba) kwa wingi.
Matunda yenye Uchachu (Citrus Fruits)
Kuchanganya ndizi na matunda yenye uchachu kama vile machungwa, Limao, au zabibu, kunaweza kusababisha kiungulia, usumbufu tumboni na mmeng’enyo mbaya wa chakula. Hii ni kwa sababu ndizi na matunda yenye asili ya uchachu yana virutubisho vya asidi na mchanganyiko huu unaweza kuwa mkali kwenye tumbo.
Vyakula vyenye wanga nyingi na protini + Parachichi.
Watu wengi huonekana wakichanganya vyakula vyao yenye mkusanyiko wa wanga na protini pamoja na Ndizi na parachichi. Ndizi na parachichi zina potasiamu nyingi, ambayo inaweza kusababisha hyperkalemia, ugonjwa unaoonyeshwa na viwango vya juu vya potasiamu katika damu. Kwa hivyo, mtu anapaswa kuzuia kuunganisha pamoja mchanganyiko huu.
Hyperkalemia inafafanuliwa kama hali ya kiwango cha potasiamu katika seramu ya damu au plasma iliyo juu ya viwango vya kawaida. Viwango vya juu vya potasiamu vinaweza kusababisha kuongezeka au kupungua kwa mapigo ya moyo, (Cardiac Arrhythmias) kitu kinacho hatarisha maisha. Kuchanganya Ndizi pamoja na Parachichi hupelekea udhaifu wa misuli, au kupooza kwa ghalfa baada ya muda flani, hii ni kutokana na kuongezeka kwa wingi wa potasiamu kwenye damu hivyo kupelekea mtu kuwa na kiwango cha juu cha Hyperkalemia.
Vyakula vyenye sukari nyingi.
Keki, cookies, Pie na cobbler, donuts, Dessert za maziwa kama vile ice cream na yoghut, Vinywaji vitamu n.k. si vizuri kuvitumia pamoja na ndizi. Kuchanganya ndizi na aina hii ya chakula kunaweza kusababisha ulaji wa sukari kupita kiasi, ambayo inaweza kuchangia kuongezeka kwa uzito, hupelekea kisukari na kuchangia shida nyingine nyingi za masuala ya kiafya.