Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viziwi kuwekewa mpango mkakati huduma za afya

Deaf Viziwi Afya Viziwi kuwekewa mpango mkakati huduma za afya

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali kupitia Wizara ya Afya iko kwenye mkakati wa kuhakikisha huduma ya afya kwa wote inawafikia watu wenye ulemavu wakiwemo viziwi popote walipo nchini.

Hayo yamesemwa jana Septemba 28, 2023 jijini Mbeya na Mratibu Huduma za Jamii Kitengo cha Tiba kutoka Wizara ya Afya, Dibogo Raymond kwenye mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu masuala yanayowakabili watu wenye ulemavu nchini.

Mafunzo hayo yanayoratibiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Duniani yanayoendelea jijini hapa.

Wiki ya Viziwi kitaifa itafikia kilele Septemba 30 mwaka huu kwenye Uwanja wa Sokoine Ruanda Nzowe- Mbeya yanalenga kutoa fursa muhimu ya ushirikishano na kujadili njia mbalimbali za kuendeleza kutambulika kwa viziwi kama jamii moja yenye lugha na utamaduni wa pekee miongoni mwa jamii kulingana na mkataba wa kimataifa wa haki na fursa kwa watu wenye ulemavu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live