Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vituo, MSD kupimwa kwa upatikanaji wa dawa aina 290

Wizarayafyapic Data Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya

Fri, 4 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Serikali ikitoa jumla ya Sh333 bilioni kwa ajili ya manunuzi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi, Serikali imesema kuanzia sasa vituo vya afya na Bohari ya Dawa (MSD) vitapimwa kwa upatikanaji wa dawa wa aina 290.

Imeelezwa kuwa hapo awali kipimo kilikuwa ni uwepo wa aina 30 ya dawa muhimu, lakini kutokana na changamoto ya malalamiko ya ufinyu wa upatikanaji dawa vituoni, kipimo sasa ni aina 290 za dawa.

Hayo yamesemwa leo Machi 4, 2022 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati akielezea utekelezaji wa wizara hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.

“Katika kuimarisha huduma za kibingwa na upatikanaji wa dawa tunaangalia

aina 290 za dawa zinazotibu magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza.

“Wananchi wanalalamika dawa hakuna kuanzia sasa tutapima upatikanaji wa dawa kwa kuangalia aina 290 za dawa na si aina 30 za dawa kama ilivyokuwa zamani,” amesema.

Waziri Ummy Bohari ya Dawa (MSD) itapimwa kwa kuangalia uwepo wa dawa za miezi mitatu.

“Tutaangalia MSD dawa aina zote 290? Na je zitadumu miezi mitatu? Mfano malaria zitatutosheleza mahitaji ya miezi mitatu? Panadol, Paracetamol tutaenda kupima hilo.

“Ngazi za vituo kuanzia hospitali zetu za halmashauri na hospitali maalum tutapima kwa kuangalia aina 290, bora useme zipo asilimia 10 kuliko kusema zipo asilimia 95 na kumbe ni aina chache za dawa na wengi wanakusanya,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live