Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vituo 208 kusajili taarifa za wagonjwa kwa alama za vidole

Vvu Etv.jpeg Vituo 208 kusajili taarifa za wagonjwa kwa alama za vidole

Sat, 8 Jul 2023 Chanzo: Mwananchi

Shirika la ICAP Tanzania limekabidhi vifaa vya Sh314 milioni vya utunzaji wa taarifa kwa kutumia alama za vidole (Biometric) na ufuatiliaji wa watu wanaohudhuria kwenye vituo vinavyotoa tiba na matunzo ya Watu wanaoishi na Virusi Ukimwi (WAVIU) mkoani Mwanza.

Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la ICAP Tanzania, Dk John Kahemele amesema vifaa hivyo vitasambazwa katika vituo vya afya 208 vinavyosimamiwa na ICAP kwenye halmashauri nane za mkoa huo. “Ugawaji wa vifaa hivyo ni utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi ambao ulitoa mwongozo wa kuboresha udhibiti wa taarifa za watu wanaoishi na VVU ambapo mbali na kurahisisha uhifadhi wa taarifa pia utaondoa matumizi ya karatasi kuhifadhi taarifa zao”

“Vifaa hivi vimetolewa chini ya Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na Ukimwi (PEPFAR) kupitia Kituo cha Marekani cha kudhibiti na kuzuia Magonjwa (CDC) ambapo tumeona tuunge mkono juhudi za Serikali kwa kuboresha mazingira ya utoaji huduma za afya,” amesema Dk John Ametaja vifaa vilivyokabidhiwa ni Kompyuta zaidi 122, vifaa vya alama za vidole (Biometric) 299, reuters za intaneti 177, zitakazosaidia kuboresha udhibiti na uhifadhi wa taarifa zao na kufuatilia mahudhurio ya matumizi ya dawa za kufubaza virusi hivyo. Mkurugenzi Mwandamizi wa Miradi CDC, George Mgomella amesema PEPFAR kupitia vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa vya Marekani nchini Tanzania ina mpango wa kutekeleza utambuzi wa kibayometriki katika vituo vya afya zaidi ya 1, 400 ifikapo mwisho wa mwaka wa fedha 2023. “Juhudi hizi zinazoendelea zitaongeza uwezo wa kuhakikisha taarifa sahihi za kufanya maamuzi kwa kudhibiti VVU, rekodi, kudhibiti upotevu wa taarifa na kuamua idadi ya uhifadhi na kudumisha faragha na usiri wa taarifa za wateja,” amesema Dk George Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Mwanza, Dk Pius Masele amesema hali ya maambukizi mkoani humo siyo ya kuridhisha huku akisema vifaa hivyo vitasaidia kufuatilia mwenendo (trend) wa maambukizi mapya na kujua hali ya mahudhurio katika kliniki za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU. Amesema takwimu zilizotolewa mwaka 2016/17 zilionyesha ongezeko la maambukizi ya VVU kutoka asilimia 4.2 mwaka 2011/12 hadi asilimia 7.2 mwaka 2016/17 ambapo asilimia 40 ya maambukizi mapya ni vijana hususani wa kike. “Juhudi zinahitajika kuongeza uelewa kwa jamii kutambua kwamba Ukimwi bado upo. Watu wachukue tahadhari ya kujilinda na hatua zenyewe ni pamoja na kuboresha mifumo ya ufuatiliaji na utunzaji wa taarifa, hii itasaidia kujua iwapo hatua zinazochukuliwa zina tija au la," amesema Dk Pius Mwenyekiti wa Waganga Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza, Dk Charles Mkombe amesema awali kutokana na matumizi ya karatasi kuhifadhi taarifa, baadhi ya taarifa za watu waishio na VVU zilikuwa zinapotea huku akidai vifaa hivyo vitaongeza ufanisi na usalama katika uhifadhi wa taarifa hizo. Naye, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi amewataka wasimamizi wa hospitali na vituo vya afya vitakavyonufaika na vifaa hivyo kuvitunza ili vilete tija na kutumika kwa muda mrefu huku, akiitaka ICAP kuendelea kuimarisha mifumo na uboreshaji wa huduma ya afya mkoani humo. "Bado kuna vituo vingine ambavyo vinahitaji msaada kama huu. Msiishie hapa endeleeni kutupigania wakati huu ambapo Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya utoaji huduma za afya nchini,”amesema Makilagi

Chanzo: Mwananchi