Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vituo 100 vya watoto njiti kujengwa nchini

Mollel Vinjiti.png Vituo 100 vya watoto njiti kujengwa nchini

Thu, 16 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema itajenga vituo 100 vya watoto njiti katika maeneo mbalimbali nchini ili kutoa huduma stahiki kwa watoto hao.

Hayo yamesemwa bungeni leo na Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Santiel Kirumba aliyetaka kufahamu mkakati wa serikali kusaidia ujenzi wa kituo cha watoto hao mkoa wa Shinyanga.

Dkt Mollel amesema Mkoa wa Shinyanga umetengewa bilioni 6 katika mwaka wa fedha 2022/23 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha watoto njiti na nchi nzima vituo vitajengwa 100.

Aidha Dkt. Mollel amemwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Bima ya afya NHIF kwamba kila mtoto atakayezaliwa njiti atibiwe kupitia bima ya mama yake.

Sambamba na hayo Dkt. Mollel amesema kwa mwaka wa fedha 2022/23 serikali imetenga shilingi bilioni 59 kwa ajili ya kukarabati vituo vya afya nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live